Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC], yatoa onyo kwa mawakala.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima. |
.NEC imewaonya wasimamizi wa uchaguzi kutotoa matokeo ya uchaguzi kwa mawakala wa chama ambao watakiuka kusaini fomu za uchaguzi namba 6 inayohusu kutunza siri za uchaguzi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima alisema kuwa lengo ni kuondoa mkanganyiko kwa baadhi ya mawakala kujitangazia matokeo kinyume cha sheria na taratibu za uchanguzi.
Amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na Miongozo katika kushughulikia mambo yote yanayohusu uchaguzi ili kuondoa malalamiko ya kucheleweshwa kwa matokeo na alisisitiza kuwa, wasiojaza fomu za siri wasipewe uwakala wa vyama vya siasa.
Kailima aliyasema hayo akifungua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Januari 22 mwaka huu, katika jimbo la Dimani, Zanzibar ambako kutakuwa na uchaguzi mdogo wa ubunge na uchaguzi wa madiwani katika Kata 20 za Tanzania Bara.
Alisema ni lazima kwa wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya katiba, sheria, kanuni na miongozo katika kushughulikia mambo yote yanayohusu uchaguzi.
Alitoa mfano kuwa, iliwahi kutoke changamoto kwa baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa kukataa kujaza fomu namba sita na kuongeza kuwa fomu ya kutunza siri ni matakwa ya kikanuni na asiyejaza asipewe uwakala wa chama cha siasa.

ZeroDegree.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC], yatoa onyo kwa mawakala.
Reviewed by Zero Degree
on
1/03/2017 08:00:00 PM
Rating: