Loading...

Pep Guardiola amewapiga marufuku wachezaji wake kula chocolate

PEP GUARDIOLA ameendelea kuwa na mbinu na mipango ambayo inaweza isiwe imezoeleka kwa watu wengi baada ya kuamua kupiga marufuku kuuzwa kwa bidhaa aina ya chocolate kwenye viwanja vya mazoezi vya Manchester City na kwenye timu za vijana.

Bidhaa hizo zenye usukari zimeonekana kutoweka rasmi kwenye maeneo hayo ya Etihad hivyo ikimaanisha viongozi na wafanyakazi wengine wenye uhitaji wa vitu hivyo wataenda kuvilia kwingine.

Chocolate zilizonunuliwa kwingine bado zinaruhusiwa maeneo hayo, hivyo wafanyakazi watatakiwa kujipanga ili kupata vyakula hivyo kama watahitaji kula.

Lakini pia mashabiki wawe na amani kwani chocolate zitapatikana uwanjani kwa ajili ya mashabiki siku za mechi tofauti. Guardiola amejipanga kuendesha mwenendo bora wa kiafya kwa wachezaji na wafanyakazi.
Sehemu ya msukumo huu inahusisha kuwapatia wafanyakazi na baadhi ya vyakula vyenye kiwango kidogo cha mafuta kama ambavyo wachezaji wanapata.

Daktari wa masuala ya lishe wa Guardiola, Silvia Tremoleda, humiza matumizi kiasi ya mafuta kwenye vyakula kama samaki, quinoa, pasta, salad, wali and kuku.

Wafanyakazi pia wametakiwa muda mrefu kujiunga na kuwa wanachama wa mazoezi (gym) na kula matunda.



Mcheza tenisi wa zamani, Tremoleda aliwahi kufanya kazi kama msimamizi wa milo wa Barcelona, na ni mwandishi mzuri na maarufu nchini Hispania.

Guardiola alianzisha kituo maalumu (camp) mwanzoni mwa msimu ambacho kilikuwepo ili kuwasaidia wachezaji kuondokana na maumbo makubwa yanayohusiana na unene.

Gael Clichy alielezea: “ukiwa na uzito mkubwa, hauruhusiwi kufanya mazoezi na timu.

“Hilo ni jambo la kwanza. Inawezekana ukawa unalisikia sana lakini kwa upande wangu hii ni mara ya kwanza nalishuhudia.

Mambo Yaliyopigwa Marufuku Ndani Ya MANCHESTER CITY:

  1. Chocolate
  2. Ngono kabla ya saa sita usiku.
  3. Pizza
  4. Kupata kifungua kinywa peke yako
  5. WiFi kwa baadhi ya maeneo
  6. Sharubati (Juisi) ya matunda
“Unatakiwa kufahamu kuwa, kama uzito wako ni kilo 60 na ukawa na uzito wa kilo 70 basi huwezi kucheza soka.”
Pep Guardiola amewapiga marufuku wachezaji wake kula chocolate Pep Guardiola amewapiga marufuku wachezaji wake kula chocolate Reviewed by Zero Degree on 3/24/2017 11:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.