Loading...

AC Milan kumng'oa Antonio Conte Chelsea?


Kuna tetesi zinaenea mitandaoni zikidai AC MILAN wanataka kumpa ofa meneja wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte.

Bosi huyo wa Chelsea anaripotiwa kuwa ndiye namba moja katika mikakati ya AC MILAN kama inavyodaiwa kwamba klabu hiyo inampango wa kubadilisha meneja kufuatia mwanzo mbaya wakiwa na Vincenzo Montella.

Kikosi cha Montella kinashikilia nafasi ya Saba kwenye msimamo wa Ligi ya Sirie A, ikiwa tayari wameshapoteza mechi Tatu kati ya mechi zao Saba za mwanzo wa msimu wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Napoli kwa poiti 9.

Wiki iliyopita Conte alisema kwamba, ki ukweli anatamani kurejea Italia, na tayari imeripotiwa kwamba Milan ndio wako mstari wa mbele sasa kutaka kumsajili meneja huyo mwenye umri wa miaka 48.

‘Nimepakumbuka sana Italia, hilo halifichiki, hivyo baada ya kupata uzoefu wa maisha nje ya mazingira ya kila siku, nitarejea,’ Conte alisema hivyo wiki iliyopita, kufuatia tetesi zilizodai kwamba anaonekana kutokuwa na mpango wa kusalia Stamford Bridge kwa muda mwingi zaidi.

Taarifa ya 'Corriere dello Sport' inadai kuwa, Milan pia wanatazamia kumrejesha Carlo Ancelotti kikosini baada ya kupoteza kibarua chake Bayern Munich siku chache zilizopita, hata hivyo, Conte anabakia kuwa chaguo lao la kwanza.

Lakini zote zinabakia kuoneka kama ni uvumi tu ukilinganisha na kauli ya Antonio Conte.
AC Milan kumng'oa Antonio Conte Chelsea? AC Milan kumng'oa Antonio Conte Chelsea? Reviewed by Zero Degree on 10/04/2017 02:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.