Loading...

Utabiri wa Antonio Conte, Chelsea vs Barcelona

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte
Antonio Conte amewaonya wachezaji wake kwamba, wanatakiwa kucheza katika kiwango cha hali ya juu sana kama wanataka kuifunga Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Conte ana amini timu yake itafanya lolote liwezekanalo ili kusonga mbele, lakini anasema kwamba watatakiwa kucheza katika kiwango cha hali ya juu kwenye michezo yote miwili.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Cobham Jumatatu baada ya droo kufanyika, Conte alisema: “Mapokezi yetu lazima yawe chanya.

“Unapokuwa kwenye hatua kama hii lazima uwe tayari kupambana na timu yoyote, na kwa suala hili lazima tuwe tayari kukabiliana na Barcelona.

“Lazima tuwe tayari kucheza nyumbani na ugenini, na haiwezekani kabisa kuiona faida ya kucheza nyumbani au ugenini katika mchezo wa kwanza.

“Unapocheza na Barcelona itakulazimu kutenga asilimia 120 katika mchezo wa nyumbani na wa ugenini kama unataka kuwa na matumani ya kusonga mbele.”
Utabiri wa Antonio Conte, Chelsea vs Barcelona Utabiri wa Antonio Conte, Chelsea vs Barcelona Reviewed by Zero Degree on 12/13/2017 05:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.