Loading...

Raia wa Zimbabwe walipa fedha kumuona Rais Mnangagwa

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa
Raia wa Zimbabwe wanaoishi katika mji mkuu wa Namibia Windhoek, wanasema wamejisikia aibu sana baada ya wao kulipishwa na ubalozi wa Zimbabwe nchini humo ili kwenda kumuona rais Emmerson Mnangagwa.

Mtandao wa habari wa Namibia, 'The Villager', ulisema kuwa wenyeji na raia wa Zimbabwe walilipa dola 16 ili kupata kiti kwenye hoteli ya Windhoek, inayoitwa Safari hotel ili kuweza kusikiliza hotuba yake.

Mtandao huo ulisema kuwa ubalozi wa Zimbambwe ulipeleka viti 300 katika eneo ambalo Bw Mnangawa alitarajiwa kuhutubia wenyeji na raia wa Zimbabwe.

Watu kadhaa waliokuwa wamekasirikia jambo hilo, walisema walizuiwa kuingia.

"Tuliambiwa tulipe lakini baadhi yetu tulizuiwa. Wengine hawakuja na wakati tuliomba kama tunaweza kuingia kwa niaba yao, lakini walikataa. Tukipiga kura hatulipi, lakini kumuona rais tunalipa."

Mwishowe wale walioingia ni wale walioweza kulipa. Inaashiria ni jinsi gani ubalozi umekubwa na uhaba wa pesa.
Raia wa Zimbabwe walipa fedha kumuona Rais Mnangagwa Raia wa Zimbabwe walipa fedha kumuona Rais Mnangagwa Reviewed by Zero Degree on 1/16/2018 06:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.