Loading...

Abdi Banda atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi


Beki wakimataifa wa Tanzania anaekipiga klabu ya Baroka FC inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini, Abdi Banda ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Aprili na Mei 2018 ndani ya timu hiyo.

Banda ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Mwezi baada ya kuisaidia timu yake kutoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya Bloem Celtic mchezo uliopigwa Aprili 28.

Beki huyo raia wa Tanzania amejinyakulia kitita cha rand 5000.00 kutoka ndani ya klabu yake ikiwa ni utamaduni wa timu hiyo kutoa kiasi hicho kwa kila mchezaji bora wa Mwezi.

Kwa sasa Baroka FC ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 34.
Abdi Banda atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Abdi Banda atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Reviewed by Zero Degree on 5/09/2018 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.