Loading...

Yanga yakiri kupitia magumu


Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imefunguka na kukiri kuwa inapitia katika changamoto kubwa kutokana na baadhi ya wachezaji mpaka kuwa majeruhi hali ambayo inawasababisha kukosa kushiriki katika michezo mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten leo Mei 09, 2018 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matayarisho yao kuelekea mtanange wao dhidi ya Tanzania Prisons mchezo utakaochezwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.

"Zipo changamoto kadhaa tunazozipitia kama timu kwa maana ya kwamba tumekuwa na wachezaji wengi majeruhi kwa muda mrefu na mpaka sasa tunaelekea ukingoni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara wapo ambao wamesharejea katika kikosi na wengine wakiwa bado hali zao hazijaimarika sana kwa maana kwamba bado hawajawa tayari kwenye kupambana", amesema Dismas.

Yanga imekwenda Mbeya ikiwa kwenye mtego wa kutoa ubingwa kwa Simba endapo itatoa sare au kufungwa kwenye mchezo huo itakuwa imevua rasmi taji la ligi kuu baada ya kudumu nalo kwa misimu mitatu mfululizo.
Yanga yakiri kupitia magumu Yanga yakiri kupitia magumu Reviewed by Zero Degree on 5/09/2018 04:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.