Loading...

Hatimaye Sugu atoka Gerezani


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya uchochezi.

Wawili hao wamepokelewa Uraiani leo Mei 10, 2018 asubuhi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho waliosafiri hadi Mbeya kwa ajili ya mapokezi hayo.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.
Hatimaye Sugu atoka Gerezani Hatimaye Sugu atoka Gerezani Reviewed by Zero Degree on 5/10/2018 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.