Loading...

Manchester United kumuuza nyota huyu kwa Vigogo wa La Liga


Manchester United wanatarajiwa kumpoteza nyota wao wa Kihispania kwa Mabingwa wa La Liga, FC Barcelona.
Wenyeji hao wa Dimba la Old Traford wanaweza kumuuza Ander Herrera kwenda Barcelona kwenye majira ya joto.

Kwa mujibu wa taarifa za usajili Uhispania, Manchester United wamejiandaa kukubali ofa ya kuanzia pauni milioni 22 kwa ajili ya kiungo huyo.
Herrera amebakiwa na miezi 12 au zaidi kidogo kwenye mkataba wake wa sasa na amekuwa akihusishwa na kuondoka baada ya kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho tangu kuwasili kwa Nemanja Matic.

Ander Herrera
Kama nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 ataondoka Manchester United kwenda Barcelona ataungana tena na Ernesto Valverde, aliyekuwa kocha wake katika klabu ya Athletic Bilbao.

Manchester United ingependelea kumbakisha Mhispania huyo baada ya kuwa wameshindwa kumshawishi Marouane Fellaini kuongeza mkataba wake.
Manchester United kumuuza nyota huyu kwa Vigogo wa La Liga Manchester United kumuuza nyota huyu kwa Vigogo wa La Liga Reviewed by Zero Degree on 5/10/2018 07:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.