Loading...

Klopp amemtaja mrithi wa Philippe Coutinho

Meneja wa Klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp
Liverpool bado haijampata mrithi wa nafasi ya Philippe Coutinho kwenye kikosi chao.
Jurgen Klopp anataka nyota mwenye ubunifu mkubwa kutoka Ligi Kuu ya Uingereza ajaze nafasi iliyoachwa na Phil Coutinho.

Mbrazil huyo alijiunga na Barcelona kwenye dirisha la usajil mwezi Januari, lakini wamefanikiwa kumaliza Ligi Kuu ya Uingereza katika nafasi nne bora, wakati huo pia wakifanikiwa kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa bila uwepo wake.

Ni wazi kwamba, umoja wa nyota wa tatu wa wekundu hao katika safu ya mbele ni bora zaidi duniani lakini Jurgen Klopp atakuwa na tamaa ya kuimarisha kikosi chake itakapowezekana, na nyota wa klabu ya West Ham United, Manuel Lanzini anaweza kuleta vionjo tofauti.

Manuel Lanzin
Kwa mujibu wa taarifa za magazeti nchini Uingereza, Liverpool bado wanavutiwa na raia huyo wa Argentina. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 amefunga magoli matatu na kutoa 'assist' 9 kwenye mechi 28 akiwa na West Ham msimu huu.


Nyinginezo:
Klopp amemtaja mrithi wa Philippe Coutinho Klopp amemtaja mrithi wa Philippe Coutinho Reviewed by Zero Degree on 5/17/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.