Loading...

Fred anayetarajiwa kujiunga na Man United aumia mazoezini

Alionekana kuwa na uchungu baada ya kifundo chake cha mguu wa kulia kufungwa bandeji
Kiungo wa kati wa Brazil Fred, anayetarajiwa kujiunga na klabu ya Manchester United amepata jeraha katika kifundo chake cha mguu katika mazoezi kabla ya kuanza kwa kombe la dunia.

United wamekubaliana kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk kwa dau la karibu pauni milioni 50, huku uhamisho huo ukitarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Daktari wa timu ya Brazil Rodrigo Lasmar alilitaja jeraha hilo lililotokea mjini London kuwa lenye maumivu makali katika mguu wake.

Fred alipata jeraha kutokana na makabiliano na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro
Brazil inaanza kampeni yake ya kombe la dunia dhidi ya Switzerland tarehe 17 mwezi Juni.

Washindi hao mara tano wa kombe la dunia baadaye watacheza katika kundi E dhidi ya Costa Rica na Serbia nchini Urusi.

Fred alijeruhiwa wakati wa mazoezi ya timu ya Brazil mjini London Uingereza
Lasmar aliongezea: kwa sasa ni mapema mno kusema chochote kuhusu hali yake. Siku ya Ijumaa tutaangalia tujue kitakachofanyikana kuamua iwapo tunahitaji kufanya uchunguzi wowote ama la.

Zinazohusiana na hii:
Fred anayetarajiwa kujiunga na Man United aumia mazoezini Fred anayetarajiwa kujiunga na Man United aumia mazoezini Reviewed by Zero Degree on 6/08/2018 05:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.