Loading...

Kocha aeleza sababu za Yanga kuvunja mazoezi


Kueleka kwenye mchezo wa Yanga na KMC kesho, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa ameamua kutumia video kuwafundisha wachezaji wake ili kupata mbinu za wapinzani.

Yanga imekuwa ikifanya mazoezi yake Uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini kwa ajili ya maandalizi ya michezo tofauti, leo haitafanya mazoezi watakuwa ndani kuangalia mechi zilizopita za KMC.

"Maandalizi yetu yapo vizuri niliwaeleza wachezaji kuwa baada ya mechi na Alliance tutaendelea na mazoezi na nitatumia video ili kuona ni jinsi gani ninaweza kuwakabili wapinzani wetu KMC siku moja tutakuwa tunaangalia michezo yao," alisema.

Yanga imefanikiwa kucheza michezo 7 kwenye ligi huku ikishinda michezo sita na kutoa sare mchezo mmoja hali iliyoifanya ijikusanyie pointi 19, itakuwa kazini kesho kucheza na KMC uwanja wa Taifa.
Kocha aeleza sababu za Yanga kuvunja mazoezi Kocha aeleza sababu za Yanga kuvunja mazoezi Reviewed by Zero Degree on 10/24/2018 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.