Mbappe aisaidia PSG kuandika rekodi hii
Paris Saint-Germain waliifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa kwa muda mrefu na klabu ya Tottenham katika historia ya soka barani Ulaya baada ya kuifunga Marseille mabao 2-0 na kufikisha ushindi wa 11 mfululizo mwanzoni mwa msimu.
Kylian Mbappe aliweka mchango wake kwa kufunga bao zuri dakika tatu tu baada ya kuingia uwanjani katika kipindi cha pili cha mchezo akitokea benchi na Julian Draxler akaihakikishia PSG ushindi kwa kutupia mpira wavuni, kwa pasi iliyotoka kwa Neymar.
Goli la 10 la Mbappe la Ligue 1 msimu huu liliiweka PSG kwenye njia ya kufikia rekodi ya ushindi wa 11 mfululizo, ambayo iliandikwa na Spurs mwanzoni mwa msimu wa 1960/61 - rekodi bora zaidi katika ligi tano bora barani Ulaya.
Meneja wa PSG, Thomas Tuchel, bila Edinson Cavani, ambaye ni majeruhi tayari alishachukua uamuzi wa kushangaza kwa kumuondoa Mbappe kutoka kwenye kikosi chake cha kwanza, kisa kikiripotiwa kuwa alichelewa mkutano wa timu hiyo kabla ya mchezo.
Mbappe alikaa benchi kwa muda wa dakika 62, kwa sehemu kubwa ya muda wote huo PSG walihangaikia ushindi dhidi ya mahasimu wao wakubwa kutoka kusini mwa Ufaransa.
Lakini goli la 38 la PSG msimu huu lilipatikana baada ya Mbappe kuingia dimbani kwenye mchezo huo kwa kiutendea haki pasi ya Angel Di Maria.
Mbappe aisaidia PSG kuandika rekodi hii
Reviewed by Zero Degree
on
10/29/2018 09:20:00 AM
Rating: