Steve Nyerere amkingia kifua Makonda
Baada ya Chama cha Waigizaji nchini (TDFAA) kueleza kutoutambua mkutano uliotangazwa kufanyika leo Januari 31, 2019 kati ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wasanii, mchekeshaji Steve Nyerere ameingilia kati akisema hakuna ukweli katika hilo.
Taarifa ya chama hicho iliyotolewa jana ilielekeza wasanii kutoshiriki kwa kuwa uongozi haukutaarifiwa, hivyo lolote litakaloamriwa lisingeweza kuwa na manufaa kwa kuwa utekelezaji wowote huanzia katika ngazi ya uongozi.
“Kulifanya jambo hili bila kushirikisha viongozi wa wana tasnia kwetu tumetafsiri kuwa ni dharau kubwa kama viongozi,” inasema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Twiza Mbarouk ambaye ni katibu mkuu.
Pia, barua hiyo ilieleza wasiwasi wa malengo ya mkutano huo ikidai kuwa wasanii wameshatumika sana kwa maslahi ya watu binafsi.
Akitolea ufafanuzi, Steve Nyerere ambaye ndiye mratibu wa mkutano wa leo amesema siyo kweli kwamba viongozi hawakupewa taarifa.
``Mkuu wa mkoa hawezi kutoka ofisini na kwenda moja kwa moja hadi kwenye tukio kama hilo bila kuwapa taarifa viongozi,`` alijibu kwa ufupi.
Katika taarifa ya mkutano huo, Steve Nyerere alisema Mkuu wa Mkoa anataka kukutana na wasanii wa fani zote katika viwanja vya Leaders Club, ili kuhakikisha wanapewa vipaumbele lakini hakuainisha katika maeneo yapi.

Chanzo: Mwananchi
Steve Nyerere amkingia kifua Makonda
Reviewed by Zero Degree
on
1/31/2019 11:05:00 AM
Rating: