Lugola: Tumeshawabaini wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya Njombe
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, alitoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma jana, alipojibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola (CCM), aliyetaka kupata kauli rasmi ya serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya kuibuka taharuki kutokana na mauaji hayo.
”Tayari tumeshawabaini watu wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji hayo kutokana na imani za kishirikina, na Naibu Waziri wangu (Hamad Yusuph Masauni) yuko huko akiendelea kuchukua hatua. Mambo yatakuwa sawa na hatutacheza na watu wanaoichokoza serikali ya Rais John Magufuli, hawatakuwa salama," alisema Lugola.
Waziri huyo alisema tangu Jumatatu, Masauni yuko mkoani Njombe ambako anafanya vikao vya ndani na kamati za ulinzi ili kujua kiini cha mauaji hayo.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mwantumu Dau Haji, alitaka kujua mpango wa serikali kuwapatia askari polisi stahili zao kutokana na baadhi ya askari kupandishwa vyeo pasi na kuwapatiwa stahiki zao.
Ajibu swali hilo, Lugola alisema Jeshi la Polisi kama ilivyo wizara na idara nyingine za serikali, lilihusika katika uhakiki watumishi, hatua ambayo ilisitisha marekebisho yoyote kwenye daftari la mishahara, ajira mpya na upandishwaji vyeo kwa watumishi wa serikali.
"Baada ya zoezi hilo kukamilika, tayari maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali zaidi ya 8,440 waliokuwa na madai mbalimbali yakiwamo stahili za kupandishwa vyeo, wamerekebishiwa mishahara na stahili zao," Lugola alisema.
Aliongeza: "Pia maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wapatao 2,143 kati ya 3,089 waliopandishwa vyeo mwezi Juni, Septemba na Desemba 2018 wamerekebishiwa mishahara yao. Hata hivyo, taratibu za kukamilisha kuwarekebishia askari waliobakia zinaendelea."

Reviewed by Zero Degree
on
1/31/2019 11:35:00 AM
Rating: