Eliud Ambokile apata shavu Afrika Kusini
Mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City ambaye pia ni kinara wa mabao kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara kwa wachezaji wa ndani, Eliud Ambokile amesajiliwa na klabu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
Mbeya City imethibitisha dili hilo kukamilika ambapo imesema, ''Nyota wa klabu yetu pendwa Eliud Ambokile amejiunga rasmi na klabu ya Black Leopards F.C ya nchini Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu''.
Black Leopards FC ni klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika kusini na ilianzishwa mwaka 1983 katika mji wa Venda uliopo kaskazini mwa Taifa hilo.
Timu hiyo inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ya huko ikiwa na alama 20 kwenye mechi 17. Imeshinda mechi 5, sare 5 na kufungwa mechi 7.
Mbeya City imemtakia heri na mafanikio Ambokile ambaye ana mabao 10 kwenye TPL akizidiwa na Makambo pekee mwenye mabao 11.

Reviewed by Zero Degree
on
1/31/2019 12:05:00 PM
Rating: