Watanzania watatu wahukumiwa kifungo cha miaka 15 Kenya kwa ugaidi
Watu hao wote ambao wanatokea Zanzibar walikamatwa mwaka jana katika Kaunti ya Wajir, upande wa Kaskazini-mashariki mwa Kenya wakijaribu kuvuka mpaka kuingia Somalia.
Ilidaiwa kwamba watu hao walikamatwa na baadhi ya vifaa ambavyo vinatumika katika vitendo vya ugaidi.
Watanzania hao wametajwa kwa majina ya Mbarouk Ali Adibu (34), Idarous Abdirahman (32) na Islahi Juma (22) na wote walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Amos Makoros na kuhukumiwa kifungo hicho wanachokitumikia katika Gereza la Wajir.
Kaunti ya Wajir imekuwa ikikabiliwa na athari za mashambulizi ya ugaidi na mara nyingi imetumika kama kituo cha kusajili magaidi kwenda kujiunga na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Ilidaiwa kwamba watu hao walikamatwa na baadhi ya vifaa ambavyo vinatumika katika vitendo vya ugaidi.
Watanzania hao wametajwa kwa majina ya Mbarouk Ali Adibu (34), Idarous Abdirahman (32) na Islahi Juma (22) na wote walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Amos Makoros na kuhukumiwa kifungo hicho wanachokitumikia katika Gereza la Wajir.
Kaunti ya Wajir imekuwa ikikabiliwa na athari za mashambulizi ya ugaidi na mara nyingi imetumika kama kituo cha kusajili magaidi kwenda kujiunga na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.
Watanzania watatu wahukumiwa kifungo cha miaka 15 Kenya kwa ugaidi
Reviewed by Zero Degree
on
1/31/2019 12:20:00 PM
Rating: