Loading...

Zahera: Gustapha anajua sana


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa ili kumfanya kiungo wake, Feisal Salum ‘Fei Toto’ awe na uwezo wa hali ya juu, atamletea kiungo mpya ambaye atampa changamoto ya kugombania namba.

Fei Toto aliyetua Yanga msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar, kwa kiasi kikubwa ndiye ambaye amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji ndani ya kikosi hicho cha Yanga. Viungo wengine ambao wanacheza sambamba na Fei ni pamoja na Papy Tshishimbi, Raphael Daud na Maka Edward.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Zahera amesema kwamba anatarajia kumpa ushindani Fei kwa kumleta kiungo Gustapha Simon kwenye timu ya wakubwa ili kutoa changamoto ya namba kwa wachezaji waliokuwepo.

“Yule mtoto (Gustapha) anajua sana na naamini akija huku timu ya wakubwa basi ataleta changamoto ya hali ya juu sana. Hawa kina Fei Toto na Tshishimbi watakuwa na kazi kubwa sana ya kugombania naye namba.

“Nilimuona alichofanya katika Kombe la Mapinduzi, ana uwezo wa hali ya juu katika kuendesha timu lakini pia kuichezesha timu, akija timu ya wakubwa basi atafanya vizuri,” alisema Kocha huyo.
Zahera: Gustapha anajua sana Zahera: Gustapha anajua sana Reviewed by Zero Degree on 1/31/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.