Mwili ulioopolewa kwenye mabaki ya ndege umetambuliwa kuwa wa Sala
Sala, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akisafiri kwenda Cardiff ikatika ndege ambayo rubani wake alikuwa ni David Ibbotson, iliyopotea mnamo Januri 12.
Mwili wake ulipatikana Jumatano baada ya kugunduliwa kwa mabaki ya ndege hiyo Jumapili asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, Polisi ya Dorset imethibitisha utambulisho wake Alhamisi usiku.
Katika taarifa yake, kikosi hicho kimesema: "mwili ulioletwa katika bandari ya leo Alhamisi Februari 7 2019, umetambuliwa rasmi kuwa wa mchezaji soka Emiliano Sala.
"Familia ya Sala na rubani David Ibbotson wamearifiwa kuhusu taarifa hii na wataendelea kupewa usaidizi na maafisa wa kitengo maalum."
"Familia ya Sala na rubani David Ibbotson wamearifiwa kuhusu taarifa hii na wataendelea kupewa usaidizi na maafisa wa kitengo maalum."
Kikosi cha uchunguzi wa ajali ya ndege awali kilieleza kwamba wakandarasi maalum wamejiunga katika operesheni hiyo, katika 'hali yenye changamoto nyingi'.
Imefanyika 'kwa heshima kubwa iwezekanavyo' na familia za wote wawili ziliarifiwa kadri shughuli zilivyokuwa zikiendelea.
Imefanyika 'kwa heshima kubwa iwezekanavyo' na familia za wote wawili ziliarifiwa kadri shughuli zilivyokuwa zikiendelea.
Mabaki ya ndege hiyo, iliyopotea wiki mbili zilizopita, yalipatikana kutoka huko Guernsey.
Mwili ulioopolewa kwenye mabaki ya ndege umetambuliwa kuwa wa Sala
Reviewed by Zero Degree
on
2/08/2019 07:08:00 AM
Rating: