TFF yajibu kuhusu uteuzi wa waamuzi mechi ya watani
Msemaji wa TFF Cliford Ndimbo amesema viingilio vitakuwa 30,000 VIP A, 20,000 VIP B na C pamoja na 7,000 kwa jukwaa la mzunguko.
Aidha amebainisha kuwa mchezo huo utapigwa jioni saa 11:00 na maandalizi yote ikiwemo suala la usalama yanaendelea vizuri hivyo mashabiki waende uwanjani tu wakatazame timu zao.
Kuhusu waamuzi watakaochezesha mchezo huo Ndimbo amesema kamati ya waamuzi itawatangaza hivi karibuni huku akipinga vikali uwepo wa hisia kuwa upangaji wa waamuzi hao umekuwa ukifanya kwa usiri.
''Niseme tu kwamba waamuzi wote hupangwa mara moja na kamati husika na sio kwamba waamuzi wa Yanga na Simba wanapangwa kwa upekee au usiri, hakuna siri yoyote na kamati ikitoa taarifa nitaituma au tutaitisha mkutano na wanahabari'', amesema.

Timu hizo zinaingia uwanjani Jumamosi zikiwa na tofauti ya pointi 22 ambapo Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 58 kileleni wakati Simba wana pointi 36 katika nafasi ya tatu.
TFF yajibu kuhusu uteuzi wa waamuzi mechi ya watani
Reviewed by Zero Degree
on
2/11/2019 09:20:00 AM
Rating: