Loading...

Maduka yafungwa kwa kuwauzia wananchi kadi za kliniki.


Tunduma. Halmashauri ya Tunduma, Mkoa wa Songwe imeyafungia maduka manne yanayotuhumiwa kuuza kadi za kliniki zenye maneno yaliyoandikwa ‘haziuzwi’.



Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Halima Mpita alisema jana kuwa, wameyafunga maduka hayo baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Tunduma kuwaamuru wanunue kadi hizo kinyume na sheria kwa watu binafsi, wakati zinapaswa kutolewa bure kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali.

Mpita alisema baada ya kupata malalamiko hayo, alituma timu ya wakaguzi kwenda kwenye maduka hayo yaliyo jirani na kituo hicho kubaini kufanyika kwa biashara hiyo haramu.

Awali, wananchi walilalamika kuuziwa kadi moja kwa Sh2,000 wakati zinapaswa kutolewa bure kwa wajawazito.

Mkazi wa Mtaa wa Sogea, Farida Sichone alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakilazimishwa kununua kadi hizo.

“Yaani ukifika pale unaulizwa una kadi? Ukiwaambia sina wanakwambia nenda duka lile pale kanunue. Tunanunua kadi hizo kwa Sh2,000. Ukiangalia kadi hizo zimeandikwa ‘haiuzwi’, lakini sisi tunaambiwa tukanunue ili tutibiwe, vinginevyo hatupati tiba,” alisema.

Aliutaka uongozi wa halmashauri hiyo kuendelea kufuatilia huduma za afya katika zahanati zinazozunguka mji huo.





ZeroDegree.
Maduka yafungwa kwa kuwauzia wananchi kadi za kliniki. Maduka yafungwa kwa kuwauzia wananchi kadi za kliniki. Reviewed by Zero Degree on 2/11/2016 05:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.