Precision Air yajitanua, sasa kutoa mafunzo kwa mafundi wake katika viwango vya kimataifa.
Dar es Salaam. Shirika la Ndege la Precision limeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo kwa mafundi wake kwa kiwango cha kimataifa lengo likiwa kupanua wigo wa kuwa na mafundi na waongoza ndege wengi nchini.
Kuanziswa kwa utaratibu huo, kumeifanya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TCAA), kulipa cheti cha ubora kwa mafundi wake pamoja na kupata cheti cha kuthibitisha ubora wa matumizi ya anga kutoka mamlaka hiyo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Prescion Air, Sauda Rajab alisema uthibitisho wa kupewa vyeti hivyo, utalifanya shirika kujitanua kibiashara kwani wafanyakazi wake wanaweza kukodishwa kwa mashirika mengine ya ndege kwa ajili ya kufanya ufundi.
Sauda alisema kuwa Oktoba mwaka jana, TCAA ililithibitisha shirika lake na kwamba kilichofanyika ni kuwasilisha mara kwa mara taarifa za utendaji wa shirika, tathmini ya utendaji na ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na taasisi za ukaguzi na uthibiti,“Tumefurahi shirika kupata cheti kutoka AOC na Amo chini ya mpango wa ukaguzi na uwasilishaji taarifa... bila kuthibitishwa kwa cheti cha AOC, huwezi kuruka na kupaki ndege zako,” alisema Sauda.
Sauda alisema bila kuwa na cheti cha Amo, ni kwamba huwezi hata kuzifanyia matengenezo ndege zako na hiyo italifanya shirika kuingia gharama kwa kutumia mafundi wa nje ya shirika. “Kwa kuwa na cheti cha Amo, tuna uwezo wa kufanyia matengenezo ndege zetu pamoja na ndege za mashirika mengine, ya ndani na nje ya nchi,” alisema.
“Tumekuwa tukifanya hivi mara kwa mara, lengo ni kupata wataalamu zaidi wa shirika sasa tunataka kupata fedha kupitia kwenye mahanga yetu, tunataka kuyabadilisha kuwa kitega uchumi kwa kutengeneza ndege nyingine mbali na zile za shirika,” aliongeza.
Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa Prescision Air, Gennaro Sicurezza, alisema kuwa shirika lina mafundi wanaoweza kutengeneza ndege za jet, ikiwamo Boeing na Airbus na kwamba wamethibitishwa na Shirikisho la Anga la Marekani na la usalama wa ndege la Ulaya.
ZeroDegree.
Precision Air yajitanua, sasa kutoa mafunzo kwa mafundi wake katika viwango vya kimataifa.
Reviewed by Zero Degree
on
2/11/2016 05:17:00 PM
Rating: