Loading...

Jibu la Hazard baada ya kuulizwa kama anahofia kupangwa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa

Eden Hazard akishangilia bao
Nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard inaonekana hatakuwa na hofu yoyote baada ya kupangwa na Barcelona kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza wamepangwa na vigogo hao wa Catalonia kwenye droo iliyofanywa leo Jumatatu, na mchezo wa pili kuchezwa  katika dimba la Nou Camp.

Lionel Messi, Suarez wakishangilia bao katika mechi yao dhidi ya Villareal
Lakini wakati akizungumza na 'BT Sport' baada ya sare ya goli 1-1 na Atletico Madrid katika mechi ya mwisho kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Jumanne iliyopita, Mbelgiji huyo hakuonyesha hofu ya kuwepo kwa uwezekano wa kumkabili Lionel Messi na wengineo.

"Hilo sio tatizo, sisi ndio Chelsea!" Hazard alimwambia mwandishi baada ya mechi hiyo iliyochezewa Stamford Bridge.

"Timu yetu ni kubwa, hivyo tunaweza kupambana na yeyote.

"Tunatambua kwamba PSG na Barcelona ni timu nzuri sana, lakini sisi ni Chelsea, hivyo tunatakiwa kuwa tayari kwa kila kitu."

Akionyesha kufurahishwa na kujiamini kwa Hazard, mwandishi alimuuliza hivi: "Unajipa nafasi ya kusonga mbele zaidi, sio?"


Kisha Hazard alijibu: "Ndio! Tunaweza kufanya kila kitu!"

Mchezo wa kwanza utachezwa Magharibi ya jiji la London mwezi Februari na wa mwisho utachezwa Catalonia mwezi Machi.
Jibu la Hazard baada ya kuulizwa kama anahofia kupangwa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Jibu la Hazard baada ya kuulizwa kama anahofia kupangwa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa Reviewed by Zero Degree on 12/11/2017 03:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.