Loading...

Borussia Dortmund wanamtaka nyota huyu wa Liverpool


Borussia Dortmund wanatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chao kwenye majira ya joto baada ya kuwa na msimu mbaya kwenye Bundesliga na Ligi ya Mabingwa. Kwa sasa wako nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi, pointi 29 nyuma ya Mabingwa Bayern Munich.

Kwa mujibu wa taarifa ya the Sun, vigogo hao wa Bundesliga wanataka kuimarisha suhemu muhimu na wanataka kusajili golikipa mpya kuweka ushindani kwa golikipa namba moja wa klabu hiyo, Roman Burki. Wanavutiwa na uwezo wa golikipa wa Liverpool, lakini watalazimika kulipia pauni milioni 10 kuipata saini yake.
Simon Mignolet alijiunga na Liverpool akitokea Sunderland kwa ada iliyoripotiwa kuwa pauni milioni 9 kwa mkataba wa miaka mitano kwenye majira ya joto mwaka 2013. Amefanikiwa kuonekana golini kwa zaidi ya michezo 200 pekee akiwa na klabu hiyo kwenye michuano yote.

Simon Mignolet
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, mara nyingi amekuwa akikosolewa kwa kuwa na kiwango kibaya tangu atue Anfield. Alikuwa na wakati mzuri katika hatua za mwanzo msimu huu lakini baada ya kufanya makosa kadhaa nafasi yake ilichukuliwa na Karius, ambaye tangu hapo amekuwa na kiwango cha kuvutia chini ya uongozi wa Jurgen Klopp.
Mbelgiji huyo hafanikiwa kupata nafasi hajafanikiwa kupata nafasi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza tangu tarehe 1 Januari, 2018 (Siku ya Mwaka Mpya) na amekuwa akihusishwa sana na kuondoka kwenye majira ya joto. Liverpool walifikiri kuhusu dili la kubadilishana na golikipa wa Stoke City, Jack Butland lakini Wafinyanzi hao wameshuka daraja na Mwingereza huyo anaonekana hana nia ya kubaki hapo.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza sasa wanataka kumuuza kwenda Dortmund na wanataka karibu pauni milioni 10, ada ambayo klabu hiyo ya Ujerumani wako tayari kulipia ili kupata saini yake.

Borussia Dortmund wanamtaka nyota huyu wa Liverpool Borussia Dortmund wanamtaka nyota huyu wa Liverpool Reviewed by Zero Degree on 5/07/2018 04:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.